Karibu Katika Kanisa La Mungu

Mstari wa Biblia ya siku

Neno la leo, Monday 8 August 2022, ni:
I had fainted, unless I had believed to see the goodness of the LORD in the land of the living. Psalms 27:13 .

 

Karibu katika tovuti ya Kanisa la Mungu la siku ya saba .Wasabato wa Kiroho.

Kanisa la Mungu ni Wakristo wanaoabudu katika siku ya saba (au Sabato, Wasabato wa Kiroho) jumuia inayochunguza Maandiko Matakatifu kwa kufuata tafasiri sahihi toka mwanzo. Falsafa yetu ya msingi ni wote wameitwa ili wapate kumwamini na kumtii Bwana Mungu na kufuata mfano wa Bwana Yesu Kristo katika Biblia. Sisi tunaheshima siku ya saba ambayo ni Sabato ya Bwana Mungu kwa sababu hizi zifuatazo kama ilivyoainishwa.

Siku ya Saba yaani Sabato ya Bwana Mungu ilikuwa mfano wa siku iliyotengwa na kutakaswa na Bwana Mungu kama siku ya ibada takatifu ya Bwana Mungu toka mwanzo yaani tangu uumbaji. Mwanzo 2:1-3. Waisraeli walikumbushwa kuweka na kuitunza siku ya saba ya Sabato ya Bwana Mungu katika amri iliyotolewa na Bwana Mungu katika Mlima Sinai. Kutoka 20:8-11; 31:12-18; Ezekeili 20:20.Bwana Yesu Kristo aliitunza siku ya saba ya Sabato wakati wa ujana wake na kutoa huduma na alijitangaza kuwa yeye Mwenyewe ndiye Bwana wa Sabato. Mark 2:27,28.Mitume ni kumbukumbu kama walivyokuta na kufanya ibada katika siku ya saba ya Sabato baada ya kifo cha Bwana Yesu Kristo. Matendo 13:14,42,44; 16:13; 17:2; 18:4.Mitume pia walitukumbusha sisi mara kwa mara kushika na kutii amri za Bwana Mungu , Yakobo anasema kuvunja amri moja ni kuvunja amri zote. Yakobo 2:10. Tunaambiwa katika Waebrania kwamba bado kuna pumziko katika siku ya saba (au siku ya Sabato). Waebrania 4:1-10.Katika kitabu cha Ufunuo kinatuambia mara tatu kanisa katika siku za mwisho watakatifu watakuwa ni hao wazikushikao amri za Mungu na imani ya Bwana Yesu Kristo, ambayo pia yana mawaidha kwa kuweka siku ya saba ya Sabato ya Bwana. Ufunuo 14:12; 12:17; 22:14.Kutoka Mwanzo hadi Ufunuo siku ya saba ya Sabato na amri za Mungu na imani ya Bwana Yesu Kristo ni kiini cha mafundisho ya mara kwa mara kwa watu wa Mungu.

Hakuna shaka yoyote kwamba Bwana Yesu Kristo anatamani wafuasi wake kujifunza Neno la Mungu. Yesu alisema: "Mwayachunguza maandiko , kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. " Yohana 5:39.

Ni lazima kutambua kutoka katika Neno la Bwana Mungu ni nini anachotarajia kutoka kwetu . Waefeso 5:10: Yaani kuenenda sawasawa na Madhumuni na Makusudi ya Bwana Mungu. Ni lazima kuishi kwa ajili ya matarajio hayo na kuwafundisha wengine. Na wala si kufuata mafundisho au mapokeo ya watu, lakini kuwa watu wa kumpendeza Bwana Mungu. Kanisa la Mungu, kama wafuasi wake, lazima kuangalia dhidi ya manabii wa uongo wa siku za mwisho. 1 Yohana 4:1-3.

Kanisa la Mungu katika mtandao tunatoa huduma ya kujitolea ajili ya kuwasaidia wale wote ambao wako tayari kwa ajili ya kutafuta ukweli wa Bwana Mungu. Sisi hatuwezi kuonyesha ukweli wa Bwana Mungu kwa kutumia kitu kingine cho chote zaidi ya Neno lake - Biblia Takatifu. Sisi tutakuwa tukitoa huduma katika mtandao , kama sehemu ya kujifunzia kama vile Biblia, kuhusiana na maswali mbalimbali na katika uchunguzi wa Maandiko Matakatifu , kutoa ushuhuda kwa wengine na kuwa viungo katika kukusaidia katika uchunguzi huu wa Maandiko Matakatifu.

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu siku ya saba ya Sabato ( kutakaswa na siku takatifu ya kupumzika ya Bwana Mungu ), mafundisho mengine ya Biblia au Biblia inasema nini kuhusu mambo mengine kama : Je, ni nini watu wa Mungu wanafundisha kuhusiana na Siku Takatifu ( Krismasi, Pasaka, sikukuu za kidini na kadhalika ). Je, muonekano na asili ya uovu nini? Kristo na Mungu ni umoja ?, Je, ni Mungu Mmoja au Ni Mungu Mmoja Mwenye nafsi tatu ? Je, asili ya Roho Mtakatifu ni nini? Jinsi gani au lini Bwana Yesu Kristo atarudi?

Kanisa la Mungu kweli linafananaje na asili yake ni nini ? Je, sheria ziligongomelewa Msalabani ? Je, Bwana Yesu Kristo alizaliwa lini ? Je, Ni Wakati gani wa Pasaka kufanyika ? Je, Siku ya Sabato ni ipi ? Jumapili, Jumamosi au siku nyingine ? Je, sisi tunahesabiwa haki kwa imani ? Je,Nini kinachotokea kati yetu wakati sisi tunapokufa ? Je, Nini hatima ya wafu ? Tutajitahidi kuonyesha majibu ya maswali hayo na mengine mengi kwa njia ya Maandiko Matakatifu katika Biblia Takatifu .